• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (4 Machi-10 Machi)

    (GMT+08:00) 2017-03-10 20:14:55

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aahidi kuunga mkono juhudi za Kenya za kupambana na ukame

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa jamii ya kimataifa itaungana kusaidia juhudi za Kenya za kukabiliana na ukame na migogoro ya kikanda.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi wiki hii, Kenya, akiwa pamoja na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta, Guterres amesema kuwa Kenya inahitaji msaada kutoka nje ili kusaidia kukabiliana na ukame ulioathiri watu milioni 3 nchini humo.

    Rais Kenyatta ameshukuru msaada wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ukame nchini humo, na kusema msaada huo utaimarisha utulivu katika jamii wakati huu ambao kuna uhaba wa maji na chakula.

    Hii ni ziara ya kwanza ya Guterres nchini Kenya akiwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, na imekuja wakati nchi hiyo ikikabiliwa na ukame mkali katika maeneo ya kaskazini ambao umesababisha mikwaruzano ya kikabila.

    Awali Guterres alizuru mji wa Baidoa, kusini magharibi mwa Somalia ambako mamilioni ya watu wanakabiliwa na njaa.

    Zaidi ya watu 100 wamefariki kwenye eneo hilo wikendi iliopita kutokana na njaa.

    Guterres amefanya mazungumzo na rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed na kutoa ombi la dola milioni $825 kwa jamii ya kimataifa ili kukabili njaa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako