Wakuu wa majeshi ya Uturuki, Russia na Marekani wajadili hatua za kuepuka migongano katika operesheni zao Syria
Makamanda waandamizi wa majeshi ya Uturuki, Russia na Marekani wamekutana nchini Uturuki kujadili njia za kuepuka migongano kwenye operesheni zao dhidi ya ugaidi nchini Syria. Makamanda hao wamebadilishana maoni kuhusu usalama wa kikanda nchini Syria na Iraq na mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria. Waziri mkuu wa Uturuki Bw. Binali Yildirim amesema mkutano huo unalenga kuimarisha uratibu kati ya majeshi ya nchi hizo tatu ili kuepuka migongano isiyotarajiwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |