Sudan yapinga dhidi agizo la Trump kuhusu wahamiaji
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ilimuitisha Alhamisi wiki hii afisa anayehusika na mambo ya nje wa Marekani mjini Khartoum ili kumueleza kuwa Sudan inapinga agizo la Donald Trump dhidi ya wahamiaji.
Agizo la Rais wa Marekani linaweka Sudan kwenye orodha ya nchi sita ambazo raia wake wameigwa marufuku kuingia Marekani, Agizo hillo lilitplewa Machi 6, 2017.
Agizo hili jipya kuhusu wahamiaji lililosainiwa Jumatatu Machi 6 na ambalo linatazamiwa kuanza kutekelezwa Machi 16 linapiga marufuku Marekani raia kutoka mataifa sita ya Kiislamu ikiwa ni pamoja na Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen, kwa kuzuiakuingia nchini humo kwa magaidi, kwa mujibu wa utawala wa Marekani.
Wizara ya mambo ya ne ya Sudan imemueleza Steven Koutsis, mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Marekani mjini Khartoum kuhusu agizo hilo la Trump kwamba haliwaridhishi.
Wizara ya mambo ya nje ya Sudan pia imemueleza mwanadiplomasia huyo wa Marekanikuwa Sudan inaitaka Marekani kuiondoa kwenye orodha yake ya nchi "zinazosaidia ugaidi."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |