Zaidi ya watu 10 wauwawa kwenye shambulizi Nigeria
Watu zaidi ya 10 wameuawa katika mashambulizi dhidi ya vijiji, kaskazini mwa Nigeria, eneo linalokabiliwa na machafuko ya makundi ya silaha.
Watu wanaoshukiwa kuwa wezi wa ng'ombe walishambuliwa vijiji vinne siku ya Jumatano katika wilaya Birnin Magaji katika Jimbo la Zamfara, linalokabiliwa na visa vya ulipizaji kisasi kufuatia mauaji ya mmoja wao aliyeuawa na wanamgambo katika jimbo hilo
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Jimbo la Zamfara Mohammed Shehu, "watu 10 waliuawa na majambazi", ambao walifyatua risasi hovyo kwa raia.
Wakazi wawili wamethibitisha mashambulizi hayo, lakini waliripoti kuwa watu zaidi 26 waliuawa.
Kwa mujibu wa mkazi mwingine akihojiwa kwa njia ya simu, Lawwali Maishanu, watu 17 waliuawa Dutsen Wake, saba Oho, mmoja Badambaji na mwengine mmoja Kabingiro.
Mashambulizi haya yalifuatiwa na mauaji ya "mwizi" aliyeuawa na wanamgambo wa Jimbo hilo katika soko siku chache zilizopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |