Aliyekuwa rais wa Maldives ahukumiwa kifungo cha miezi 19 gerezani
Mahakama ya jinai nchini Maldives wiki hii imemhukumu aliyekuwa rais wa nchi hiyo Maumoon Abdul Gayoom kifungo cha miezi 19 gerezani kwa kosa la kuzuia utekelezaji wa sheria.
Mahakama hiyo pia imemhukumu jaji mkuu wa Mahakama Kuu ya Maldives Abdulla Saeed na jaji Abdullah Yameen kifungo cha miezi 19 kwa kosa hilohilo.
Watu hao walipokamatwa na polisi, walikataa kukabidhi simu zao. Gayoom amesema idara ya uendesha mashtaka haiwezi kuthibitisha kuwa upo ushahidi wa kutosha kwenye simu zao.
Habari nyingine zinasema, watatu hao bado wanakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kupindua serikali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |