Rais wa Zimbabwe ajaza fomu za kugombea katika uchaguzi mkuu ujao
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amewasilisha fomu za kuteuliwa kugombea nafasi ya urais kupitia chama tawala nchini humo ZANU-PF katika uchaguzi utakaofanyika Julai 30 mwaka huu.
Rais Mnangagwa amekuwa mgombea wa kwanza wa chama hicho kugombea nafasi ya urais baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe kujiuzulu mwezi Novemba mwaka jana baada ya jeshi kuingilia kati, hivyo kumaliza miaka 37 ya rais huyo kuwa madarakani.
Mpinzani mkubwa wa Mnangagwa, kiongozi wa Muungano wa MDC, Nelson Chamisa, pia amewasilisha fomu zake kwenye Mahakama ya Uteuzi. Wagombea wengine watatu wa nafasi hiyo ni pamoja na aliyekuwa makamu wa rais na kiongozi wa chama cha NPP Bi. Joyce Mujuru ambaye naye amewasilisha fomu zake kwenye mahakama hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |