Mgogoro wa wahamiaji watokota Italia
Serikali ya Italia imefutilia mbali ziara ya waziri wake wa uchumi kwenda nchini Ufaransa kufuatia mgogoro wa uhamiaji baina ya nchi hizo mbili.
Italia imekua na hasira tokea Rais Macron wa Ufaransa alipoituhumu kwa kutohusika kutoa msaada wowote kwa mamia ya wakimbizi wanaoingia Italia.
Waziri wa mambo ya ndani wa Italia Matteo Salvini alisema katika mkutano kuwa hakutakua na ziara yoyote nchini Ufaransa mpaka nchi hiyo itakapoomba radhi juu ya matamshi hayo.
Bwana Salvini hakuwa tiyari kuzungumzia suala hilo kwa nchi ambayo mara kadhaa imekua ikiwazuia wahamiaji kuingia katika mipaka yake.
Mapema Kansela wa Austria Sebastian Kurz alisema watafanya kila liwezekanalo kuzuia wahamiaji haramu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |