• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Juni 9-Juni 15)

    (GMT+08:00) 2018-06-15 19:03:02

    Trump akutana na Kim Jong Un

    Mkutano wa kihistoria kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un umefanyika nchini Singapore.

    Wawili hao walikutana kwanza kwa dakika 38 kwa mujibu wa ikulu ya White House, na walikuwa ni wawili hao pekee na wakalimani wao.

    Mkutano huo ulianza kwa viongozi wawili kusalimiana kwa tabasamu na kisha kuelekea ukumbi wa maktaba ya Cappela Hotel kwa ajili ya sehemu ya kwanza ya mkutano wa ana kwa ana baina yao.

    Bw Trump amesema wawili hao walipiga hatua kubwa na kwamba karibuni kutakuwa na sherehe ya kutia saini nyaraka ya makubaliano.

    Wamekuwa wakijadiliana kuhusu njia za kupunguza uhasama rasi ya Korea na kati ya Korea Kaskazini na Marekani na pia jinsi ya kupunguza silaha za nyuklia.

    Baadaye walitia saini waraka wa makubaliano.

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema, anatarajia Korea Kaskazini itapata maendeleo makubwa katika kupunguza silaha za nyuklia ndani ya miaka miwili na nusu ijayo.

    Bw. Pompeo ambaye akiwa ziarani nchini Korea Kusini, wiki hii amesema, rais Donald Trump wa Marekani ameeleza wazi kuwa, ahadi yake ya kusimamisha mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini itatekelezwa kama mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini yataendelea vizuri.

    Bw. Pompeo pia amesema, makubaliano yaliyofikiwa na Marekani na Korea Kaskazini hayakuonekana kwa kikamilifu kwenye taarifa ya pamoja, ikimaanisha kuwa juhudi nyingine nyingi zinahitajika kufanyika katika siku za baadaye.


    1  2  3  4  5  6  7  8  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako