Watu 103 wakamatwa katika maandamano ya kupinga kukamatwa Bobi Wine Uganda
Polisi nchini Uganda inasema imewakamata watu 103 katika maandamano yaliozuka kupinga kukamatwa kwa mbunge wa upinzani Robert Kyagulanyi au Bobi Wine pamoja na wabunge wengine kadhaana wanaharakati nchini Uganda.
Inaarifiwa pia mtu mmoja ameuawa katika purukushani hiyo.
Vikosi vya usalama nchini Uganda vilizima maandamano kwenye mji mkuu hapo Kampala kupinga kukamatwa kwa Bobi Wine .
Waandamanaji wamechoma moto magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani.
Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria.
Wengi wanayaona mashataka hayo kama yaliyochochewa kisiasa.
Lakini wakati huo huo Jeshi la Uganda limeomba msamaha baada ya askari wake kuonekana kwenye mkanda wa video wakimpiga mwandishi wa habari kwenye maandamano hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |