Pande za Sudan Kusini zasisitiza ahadi ya pamoja ya kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani
Pande mbalimbali zinazojihusisha na mchakato wa amani wa Sudan Kusini, zimewasisitizia watu wa nchi hiyo kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani ya Khartoum.
Ahadi hiyo imo kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa na Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD.
Pande hizo pia zimeapa kuendelea na juhudi za kutafuta umoja, amani na ustawi katika msingi wa haki, usawa na kuheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria.
Taarifa pia imesisitiza kuwa vita na mapambano nchini Sudan Kusini vimesababisha mateso yasiyoelezeka kwa watu wa nchi hiyo, na kuharibu jamii ya nchi hiyo.
Mwishoni mwa mwezi uliopita pande zinazopambana nchini humo zilisaini Makubaliano ya Amani ya Khartoum nchini Sudan, ukiwemo usitishaji vita wa kudumu ulioanza kutekelezwa ndani ya saa 72.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |