Kofi Annan, aaga dunia akiwa na miaka 80
Wiki hii dunia imeendelea kuoboleza kufariki kwa aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ambaye aliaga dunia akiwa na miaka 80.
Annan alikuwa ni mwafrika mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, akihudumu mihula miwili kuanzia mwaka 1997 hadi 2006.
Baadaye akahudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria na kuchangia kupatikana kwa suluhu la amani la mzozo wa nchi hiyo.
Katika taarifa iliyotangaza kufariki kwake, wakfu wa Kofi Annan ulimtaja kama mtu aliyejitolea sana katika masuala ya kimataifa mbaye katika maisha yake yote alipigania kuwepo ulimwengu wenye amani.
Muhula wa Annan kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ulikumbwa na vita vya Iraq na janga la virusi vya HIV na Ugonjwa wa ukimwi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |