Idadi ya vifo kutokana na kubomoka kwa daraja Italia yafikia 43
Kazi ya uokoaji baada ya daraja kubomoka kwenye eneo la Genoa, Italia, imemalizika na idadi ya vifo kutokana na ajali hiyo imefikia 43.
Taarifa iliyotolewa Jumapili na serikali ya mji wa Genoa imesema mbali na waItalia, wahanga wengine wanatoka Albania, Colombia, Chile, Ufaransa, Jamaica, Romania na Peru.
Serikali ya Italia imetangaza hali ya dharura ya miezi 12 kwenye eneo la Liguria, ili kurahisisha kazi ya uokoaji na ukarabati.
Hivi sasa serikali kuu ya Italia imetenga Euro zaidi ya milioni 30 kwa ajili ya sehemu hiyo, ambazo zitatumiwa kujenga barabara mbadala na kuwapanga wakazi wa eneo hilo waliohamishwa kutokana na ajali hiyo.
Tarehe 14 mwezi huu, daraja la Morandi lililoko kwenye sehemu ya Genoa lilibomoka wakati magari takriban 30 yanapita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |