Utafiti waonesha asilimia 48 waingereza wanaunga mkono kufanyika tena kura ya maoni ya Brexit
Uchunguzi mpya uliofanywa na gazeti la Independent la Uingereza umeonesha kuwa asilimia 48 ya wahojiwa wanaunga mkono kufanyika tena kwa kura za maoni kuhusu Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 4 kuliko wiki nne zilizipita. Asilimia 24 tu ya wahojiwa walipiga kura ya hapana.
Uchunguzi huo umeonesha kuwa mpango wa Brexit uliotolewa na waziri mkuu Bibi Theresa May umeleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama chake, na pia haukukubaliwa na Umoja wa Ulaya, hali ambayo imetia wasiwasi wananchi wa Uingereza.
Hivi sasa watu zaidi ya laki sita wameitikia ombi lililotolewa na gazeti la Independent la kufanya tena kura ya maoni kuhusu Brexit.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |