• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 3-Novemba 9)

    (GMT+08:00) 2018-11-09 16:06:55

    Uganda yaanza kutoa chanjo ya Ebola kwa wafanyakazi wa afya wenye hatari ya kuambukizwa

    Uganda imeanza kutoa chanjo ya homa ya Ebola kwa wafanyakazi wa afya walioko kwenye maeneo yenye maambukizi ya ugonjwa huo kwa kusaidiwa na Shirika la Afya Duniani WHO.

    Mjumbe wa WHO nchini Uganda Bw. Yanas Woldemariam amesema zoezi hili limeanza kwenye sehemu ya Ntoroko magharibi mwa Uganda. Ntoroko ni moja kati ya sehemu tano zenye hatari zaidi ya kuambukizwa zilizoko mpakani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na hivi sasa wafanyakazi wasiopungua 3,000 wa afya wanatoa huduma za kukinga Ebola katika sehemu hizo.

    Bw. Woldemariam amesema Uganda imepiga hatua kubwa katika kupunguza hatari ya kuambukizwa kwa wafanyakazi wa afya, na chanjo hiyo inafanya kazi na itawalinda vizuri.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako