Ajali za bodaboda husababisha vifo vya watu 800 kila mwaka Tanzania
Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Tanzania Bw Hamad Masauni amesema tangu mwaka 2008, watu wasiopungua 800 wanapoteza maisha yao kila mwaka kutokana na ajali za barabarani zilizohusisha bodaboda nchini Tanzania.
Amesema tangu mwaka 2008 hadi mwezi Septemba mwaka huu, idadi ya ajali za barabarani zilizohusisha bodaboda na bajaji imefikia elfu 38 na watu 8,237 wamefariki katika ajali hizo, wengine 37,521 wamekuwa walemavu, yaani watu wasiopungua 823 wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na ajali za bodaboda nchini humo.
Mbali na hayo, amezungumzia suala la madereva wa magari ya serikali wanaokiuka sheria za usalama barabarani, na kuwaamuru makamanda wa polisi kuwakamata madereva hao, na kufikishwa mahakamani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |