Afrika Kusini kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji
Kongamano kuhusu uwekezaji nchini Afrika Kusini limefanyika jana mjini Shanghai, China. Waziri wa biashara na viwanda wa Afrika Kusini Bw. Rob Davis amesema Afrika Kusini inatumai kupitia kongamano hilo kuonyesha kwa pande zote sura ya taifa ya Afrika Kusini na uwezekano wa uwekezaji, na inatumai kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji ili kutoa urahisi zaidi kwa kampuni na wawekezaji wa China. Amesema :
"Rais Cyril Ramaphosa ametangaza mpango wa kuvutia uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 100 ndani ya miaka mitano ijayo. Tuna imani kupitia kuboresha zaidi mazingira ya uwekezaji kutimiza lengo hilo, na kuleta maendeleo ya kasi zaidi ya uchumi wa Afrika Kusini, ili kukabiliana changamoto tulizokabiliwa nazo katika kujiendeleza."
Bw. Rob Davis pia amesema, baada ya kuongezeka kwa ushirikiano na biashara kati ya China na Afrika Kusini, mustakabali wa uwekezaji wa China nchini Afrika Kusini utakuwa mzuri zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |