• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 3-Novemba 9)

    (GMT+08:00) 2018-11-09 16:06:55

    Umoja wa Mataifa watoa wito wa kufanya upigaji kura wenye amani na kuaminika nchini Somalia

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Bw Nicholas Haysom, jana ametoa wito kwa pande husika zifikie makubaliano kuhusu kufanya uchaguzi wa urais kwa amani na wenyewe kuaminika kwenye jimbo la kusini magharibi mwa Somalia.

    Ametoa taarifa akisema tofauti kati ya pande husika zinaweza kusababisha vurugu kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 17 mwezi huu. Uchaguzi huo ni wa kwanza kwenye mchakato wa chaguzi mfululizo zitakazofanyika katika siku zijazo nchini humo, hivyo ni muhimu kuufanya uchaguzi huo uwe mfano mzuri kwa mchakato wa uchaguzi wa amani na wenye kuaminika.

    Ametoa wito kwa pande husika zifanye juhudi kwa pamoja, ili kuhakikisha mchakato wa uchaguzi nchini Somalia unaendelea kwa kufuata kanuni.


    1  2  3  4  5  6  7  
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako