Watu 900 wameuawa ndani ya siku tatu mwezi uliopita DCR.
Wiki hii Umoja wa mataifa umetoa ripoti kwamnba vita vya kikabila magharibi mwa Jamahuri ya Kidmeokrasi ya Congo vimesababisha vifo vya takriban watu 890 katika muda wa siku tatu mwezi uliopita.
Umoja huo unasema mapigano kati ya jamii za Banunu na Batende yalizuka katika vijiji vinne huko Yumbi, na kwamba idadi kubwa ya wakakaazi wa eneo hilo wameyatoroka makwao.
Uchaguzi mkuu wa Desemba 30 uliahirishwa huko Yumbi kutokana na ghasia.
Mashambulio hayo yanaarifiwa kutokea kuanzia Desemba 16 hadi 18.
Nyumba 465 na majengo yaliteketezwa au kuharibiwa, zikiwemo shule mbili za msingi, kituo cha afya, soko na ofisi ya tume huru ya uchaguzi katika eneo hilo, Umoja huo umesema.
Raia walioachwa bila ya makaazi ni pamoja na watu 16,000 waliotafuta hifadhi kwa kuvuka mto Congo hadi katika nchi jirani ya Congo-Brazzaville, umeongeza.
Ripoti zinaashiria mapigano yalizuka wakati watu wa kabila la Banunu walipojaribu kumzika mojawapo ya viongozi wao wa kitamaduni katika ardhi ya kabila la Batende.
Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi alitangazwa mshindi lakini mpinzani mwingine wa utawala wa sasa, Martin Fayulu, anasisitiza yeye ameshinda, na kutuhumu Tshisekedi wameingia katika makubaliano na rais anayeondoka Joseph Kabila.
Wiki hii mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ambaye ni Rais wa Rwanda Paul Kagame ameita kikao maalum na baadhi ya viongozi barani humo ili kujadili hali ya mapigano na uchaguzi huo wa DRC.
Akihutubia ufunguzi wa mkutano huo rais Kagame amewapongeza viongozi wa SADC kwa juhudi zao katika kukabiliana na mgogoro baada ya uchaguzi nchini DRC, na kusisitiza haja kwa waafrika kukutana na kutafuta kwa pamoja ufumbuzi wa matatizo yao.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |