Ali Bongo arejea nyumbani
Rais wa Gabon Ali Bongo yuko nyumbani nchini Gabon tangu Jumatatu baada ya kuendelea kupewa matibabu kwa siku kadhaa nchini Morocco.
Taarifa ya kurejea kwa rais ali Bongo nchini Gabon imethibitishwa na runinga ya taifa ya Gabon pamoja na familia yake.
Familia yake imesema madaktari wamebaini kwamba safari ya rais Ali Bongo kwenda Gabon si hatari kwa afya yake..
Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia 24 Oktoba kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.
Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.
Rais Ali Bongo alichukua madaraka ya kuiuongoza nchi hiyo kutoka kwa babab yake Omar Bongo mwaka 2009, ambaye aliiiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa zaidi ya miaka 40.
Rais Ali Bongo anarejea nchini diku chache baad aya utawala wake kuponea kuangushwa kufuatia jaribio la mapinduzi lilitibuliwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |