Wapiganaji 800 wenye silaha wamekamatwa nchini Ethiopia wakati hali ikiendelea kuwa ya wasiwasi
Serikali ya Ethiopia imesema imewakamata waasi 835 wenye silaha katika wiki kadhaa zilizopita wakati hali ya wasiwasi ikiendelea kuongezeka kwenye maeneo mbalimbali ya jimbo la Oromia.
Kituo cha uongozi kilichoanzishwa na serikali ya Ethiopia kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara kwenye majimbo ya Oromia na Benishagul Gumuz, kimesema waasi waliokamatwa ni wapiganaji wa kundi la Oromo Liberation Front. Kituo hicho pia kimekanusha uvumi kuwa jeshi la anga la nchi hiyo limefanya mashambulizi kwenye jimbo la Oromo.
Taarifa iliyotolewa na kituo hicho baada ya ripoti zinazotolewa na wanaharakati na vyombo vya habari vya nje, kuwa jeshi la anga la Ethiopia lilifanya mashambulizi dhidi ya vituo vya kundi la Oromo Liberation Front. Kamanda wa jeshi la anga la Ethiopia Brigedia Jenerali Yilma Merdasa amesema ripoti hizo si za kweli na zina nia mbaya ya kuvuruga amani na usalama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |