China yaitaka Canada kuheshimu mamlaka ya kisheria wa China
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, baada ya kuridhishwa na ushahidi, mtuhumiwa wenye uraia wa Canada Robert Lloyd Schellenberg amehukumiwa kifo kutokana na kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, na kwamba baadhi ya watu husika wa Canada wanaopinga hatua hiyo wanakosa moyo wa kimsingi wa sheria.
Hivi karibuni baada ya Schellenberg kuhukumiwa kifo, waziri mkuu wa Canada Bw. Justin Trudeau alilalamika kuwa hukumu hiyo haifuati utaratibu wa kisheria, huku akisema serikali ya Canada inafuatilia tukio hilo.
Bibi Hua amesisitiza kuwa mtuhumiwa huyo ameshiriki katika uhalifu wa kimataifa wa biashara haramu ya dawa za kulevya na kusafirisha kilo 222.035 za dawa hizo aina ya methamphetamine.
Mahakama imemkuta na hatia ya kupokea dawa hizo Oktoba 14 kutoka mkoa wa Guangdong kusini mwa China akiwa anajiandaa kuzisafirisha kwenda Australia.
Mwezi Novemba mahakama hiyo ilimhukumu kifungo cha miaka 15 gerezani, na kumtaka alipe dola elfu 22 na kujiandaa kufukuzwa nchini, lakini alikata rufaa.
Baadaye mahakama ya mkoa wa Liaoning ilitaka kesi hiyo isikilizwe upya kutokana na adhabu iliyotolewa kuwa ndogo. Ushahidi zaidi uliwasilishwa mahakamani kabla ya hukumu hiyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |