Shirika la fedha la kimataifa IMF limepunguza kwa kiwango kikubwa makadirio yake ya ukuaji wa uchumi duniani kwa mwaka huu. IMF imesema hali hiyo inatokana na kuathirika kwa uchumi iliyosababishwa na janga la corona.
IMF inakadiria kuwa uchumi wa dunia utanywea kwa asilimia 4.9 mwaka huu, ikiwa ni hali mbaya zaidi kuliko ilivyokadiriwa hapo mwezi Aprili kwamba uchumi ungepungua kwa asilimia 3.
IMF inakadiria kuwa pato jumla la taifa kwa nchi 19 za Umoja wa Ulaya zinazotumia sarafu ya Euro, litapungua kwa asilimia 10.7 mwaka huu. IMF imesema Marekani taifa lenye uchumi mkubwa duniani litakabiliwa na kupungua kwa pato lake jumla la taifa hadi asilimia 8 katika mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |