Rais wa Uganda aonya kurejesha hatua za zuio dhidi ya COVID-19
Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameonya kuwa kama maambukizi ya COVID-19 na idadi ya vifo vitaongezeka, hatua za zuio zitarejeshwa.
Akihutubia kwa njia ya televisheni, Rais Museveni amesema, kama raia hawatafuata hatua za kinga zilizoagizwa, na kama nchi hiyo itaingia kwenye kipindi cha hatari zaidi, basi atalazimika kurejesha hatua za karantini ili kuzuia kuenea kwa virusi.
Amesema nchi kadhaa zimerejesha hatua za zuio kutokana na watu kutofuata vizuri hatua za kinga na kuongezeka kwa hali ya maambukizi, na waganda wanapaswa kuepeuka hali hiyo.
Vilevile rais Museveni amewahimiza waganda wavae barakoa kwenye maeneo ya umma, kunawa mikono kwa sabuni na kudumisha mazingira safi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |