Marekani hali tete, Idadi ya maambukizi ya Corona yafikia milioni 9.3 duniani
Wataalam wa afya nchini Marekani wametahadharisha kwamba hospitali za nchini humo zinaweza kukabiliwa na wingi wa wagonjwa wa COVID 19 kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona katika siku za hivi karibuni nchini humo.
Majimbo yaliyokumbwa zaidi na ongezeko la maambukizi ya Corona ni Florida, Texas miongoni mwa majimbo mengine.
Wakati huo huo Brazil imethibitisha kuwa na maambukizi mapya 40,700 huku idadi mpya ya vifo ikiwa ni zaidi ya watu 1,100. Zaidi ya watu milioni 9.3 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona ulimwenguni kote. Watu zaidi ya 481,000 wamekufa kutokana na COVID -19.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |