Tedros: Idadi ya wagonjwa wanaothibitishwa kuambukizwa Corona yakadiriwa kufikia milioni 10 katika wiki ijayo
Katika mkutano wa waandishi wa habari wa kawaida wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Tedros amesema kuwa zaidi ya wagonjwa milioni 9.1 waliothibithshwa kuambukizwa virusi vya Corona wameripotiwa duniani kote, na watu 470,000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo.
Katika mwezi wa kwanza wa janga hilo, kulikuwa na kesi chini ya elfu kumi. WHO inakadiria kwamba idadi ya wagonjwa wanaothibitishwa kuambukizwa Corona itafikia milioni 10 katika wiki ijayo.
Aidha Tedros Ghebreyesus alisema, virusi vya Corona vitaenea kwa kasi zaidi, na athari zake zitadumu kwa miaka zaidi ya kumi.
Bw. Tedros amesema hayo wakati alipohudhuria mkutano wa afya kwa njia ya video.
Pia amesema, tishio kubwa zaidi linaloikabili dunia sio virusi, bali ni ukosefu wa mshikamano na uongozi wa dunia nzima.
Ameongeza kuwa katika dunia inayogawanyika, hatuwezi kushinda virusi hivyo. Hakuna yeyote atakayekuwa salama kabla ya sote kuwa salama.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |