Caf yamuweka chungu kimoja Mbwana Samatta na mkali wa Chelsea, Didier Drogba
Shirikisho la soka Barani Afrika Caf, limemtaja mshambuliaji hatari wa Taifa Stars ya Tanzania na klabu ya Aston Villa kutoka Premier League, Mbwana Samatta kuwa ni mingoni mwa wachezaji wanne kutoka Afrika wenye uwezo wa hali ya juu kabisa katika matumizi ya vichwa wawapo uwanjani.
Caf imesema kuwa Afrika imebahatika kushuhudia wapiga vichwa wazuri kwenye soka, baadhi yao ni pamoja na aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba.
Flávio da Silva Amado ambaye alikuwa striker wa timu ya taifa ya Angola na klabu ya Atlético Petróleos de Luanda kutoka huko huko, huku Caf ikimtaja wa nne kuwa ni Mfarao, Hossam Hassan mkali huyu wa zamani wa klabu ya Zamalek.
Shirikisho hilo lenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya soka Barani Afrika limemuweka Mbwana Samatta mwenye jumla ya magoli 31 aliyofunga kwa kutumia kichwa nafasi ya pili kwa uwezo wake wa kutumia mipira ya vichwa baada ya Didier Drogba waliyemuandika kama mchezaji wa kwanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |