• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vivutio vya Anshun, mkoani Guizhou

    (GMT+08:00) 2008-12-29 16:51:12

    Anshun ya mkoani Guizhou, iliyoko sehemu ya kusini magharibi mwa China ni mahali penye vivutio vingi vya milima na mito. Huko kuna poromoko maarufu la maji la Huangguoshu, sura ya ajabu ya ardhi ya Karst pamoja na mila na desturi ya kipekee ya makabila madogo.
    Anshun iko kwenye uwanda wa juu wa Guizhou ulioko sehemu ya kusini magharibi mwa China. Maana ya maneno ya Anshun ya Kichina ni neema, baraka na yenye hali ya hewa nzuri. Tunapotaja Anshun, hatuna budi kueleza kuhusu poromoko kubwa la maji la Huangguoshu. Naibu meya wa mji wa Anshun, Bw. Fu Youxin alisema,
    "Poromoko la maji la Huangguoshu siyo la kwanza kwa ukubwa duniani. Lakini ninaweza kusema, hilo ni poromoko la maji linalopendeza zaidi duniani. Kiasi cha miaka 380 iliyopita, msomi maarufu wa zama za kale nchini China Xu Xiake alivutiwa sana na mandhari hiyo nzuri, akasema, maji meupe kama pamba yanayochipuka kwa mbali, na upinde wenye rangi mbalimbali kama kitambaa cha hariri cha kupendeza. Anshun ni mahali penye maporomoko mengi. Mbali na hayo, tuna poromoko kubwa la maji la Toupotan, poromoko zuri la maji la Yinlianzhuitan, yote ni ya kupendeza na kuvtia sana. Kwenye eneo la Anshun kuna maporomoko ya maji zaidi ya 110."


    1 2 3 4 5
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako