• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vivutio vya Anshun, mkoani Guizhou

    (GMT+08:00) 2008-12-29 16:51:12

    Wapendwa wasikilizaji, mnayosikia sasa ni sauti ya maji kwenye poromoko la maji la Doupotang, ambalo liko kwenye umbali wa kilomita 1 kutoka poromoko la maji la Huangguoshu lililoko sehemu ya juu ya mtiririmko wa mto, poromoko hilo la maji lina umbali wa mita 21, poromoko hilo la maji ni pana zaidi kati ya maporomoko ya maji ya Huangguoshu. Kwenye sehemu ya juu ya poromoko la maji la Doupotang kuna bwawa la maji la mawe ya chokaa lenye eneo la mita za mraba elfu 15. Poromoko la maji la Doupotang ni ya ajabu sana, kila yanapofika mafuriko ya maji, husikika sauti kubwa ya ngurumo, hivyo watu wanaliita poromoko la maji la Doupotang kuwa ni "poromoko la maji la ngurumo". Mwongozaji wa watalii Dada Liao alisema,
    "Poromoko la maji la Doupotang ni pana zaidi kati ya maporomoko ya maji ya Huangguoshu, ambalo lina upana wa mita 105 na urefu wake kwenda juu ni mita 21. Sehemu ya mwisho ya sinema iitwayo "Safari ya Magharibi" ilipigwa huko. Hili ni poromoko la maji lililo pana zaidi kati ya maporomoko ya maji ya Huangguoshu, na ndani yake mna bustani ya "Ndege 100", ambamo licha ya tausi, kuna ndege wengine kama bata mzinga, bata mwitu na Yuanyang. Huko pia kuna mimea ya aina nyingi. Tuliwahi kufika kwenye mto Baishui, tena tulifika kando ya mto, tulifurahi sana."


    1 2 3 4 5
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako