• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vivutio vya Anshun, mkoani Guizhou

    (GMT+08:00) 2008-12-29 16:51:12


    Dada Peng kutoka mkoa wa Sichuan ni mara ya kwanza kufanya matembezi kwenye sehemu ya Huangguoshu. Alisema, alishangazwa sana na mandhari nzuri ya Huangguoshu. Akisema:
    "Hivi sasa ni majira yenye mvua nyingi, hivyo maporomoko ya maji yanapendeza zaidi kuliko wakati mwingine, ninaposimama karibu na sehemu ya chini ya poromoko la maji, ninaona kama inanyesha mvua ya rashasha, ninasikia raha sana. Sehemu nyingine zenye mandhari nzuri, hazina hali hiyo."
    Sehemu ya mandhari ya Huangguoshu imejulikana sana nchini China na katika nchi za nje kutokana na kuweko maporomoko mengi ya maji, na inasifiwa kuwa ni "poromoko la maji la kwanza nchini China". Wakati inapozungumziwa sehemu ya mandhari ya Huangguoshu, naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi, Bw. He Xiaoyun alifurahi sana. Alisema:
    "Kundi la maporomoko ya maji ya Huangguoshu lina maporomoko ya maji 18 yenye umaalumu tofauti, yakiwemo maporomoko makubwa ya maji, ya umbo la ajabu, hatari na yenye umbo zuri, ambayo yameorodheshwa katika rekodi ya Guinness. Hapa pia ninawaalika marafiki wote wende kushuhudia maporomoko ya Huangguoshu. Ni hakika kuwa mtakuwa na safari ya furaha."
    Kwenye eneo la Huangguoshu lenye kilomita za mraba kumi kadhaa, kuna milima mingi ya kupendeza, mapango ya mawe ya chokaa na vijito vingi. Licha ya kuweko maporomoko mazuri ya maji ya Huangguoshu, huko pia kuna jumba zuri la dragon. Naibu meya wa mji wa Anshun, Bw. Fu Youxin alisema,
    "Hapa unaweza kuburudishwa na maziwa ya kimaumbile ya China. Ukitembea kwa mashua ndani ya pango la mawe ya chokaa, unaweza kushuhudia maji yanayotoka kwa nguvu pamoja na mawe ya chokaa yenye maumbo mbalimbali ya ajabu. Anshun ina mapango mengi ya ajabu kwenye eneo hilo la milima lenye kilomita za mraba karibu elfu 10, idadi ya mapango inazidi 1,200 yakiwemo mapango maarufu zaidi ya jumba la dragon na pango la Yelang."


    1 2 3 4 5
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako