Wapendwa wasikilizaji, endapo utafika Anshun mkoani Guzhou, licha ya kuangalia mandhari nzuri ya kimaumbile, utashuhudia mila na desturi ya watu wa makabila madogo madogo. Ofisa mwenezi wa mji wa Anshun, Bi. Yna Xueli alisema,
"Mji wa Anshun una makabila madogo 39 yakiwemo ya Wabuyi, Wamiao, Wahui na Wageilao. Watu wa makabila madogo wana siku kuu nyingi. Kwa mfano, siku kuu ya Tiaohua ya kabila la Wamiao, ambayo ni ya kwanza kuadhimishwa kwa sherehe kubwa, na ni siku kuu ya jadi iliyoanza zamani zaidi. Inasemekana, siku kuu hiyo ilianzishwa na shujaa Yang Nu wa kabila la Wamiao. Maana ya Tiaohua ni kucheza ngoma pembezoni mwa mti wa maua uliopo kwenye mtelemko wa mlima. Watu wa kabila la Wamiao wanaiita Tiaohua kuwa ni Oudao, maana yake ni sherehe kwenye mtelemko wa mlima. Kila inapofika siku kuu hiyo, watu wa kabila hilo, hususan vijana wanavaa nguo za sikuu kuu, wanaume wanapiga ala ya muziki ya Lusheng, wanawake wanatingisha makengele na kutupa leso, huku wakicheza ngoma kwa kuuzungushia mti wa maua, licha ya hayo, kuna mchezo wa kukwea mlingoti, mashindano ya ufundi wa ushonaji, maonesho ya Wushu na mchezo wa kupiganisha mafahali.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |