• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujifurahishe kwa mandhari ya theluji mkoani Jilin

    (GMT+08:00) 2009-01-12 15:30:12

    Baada ya kuingia majira ya baridi, hususan katikati ya mwezi Novemba, theluji zinatokea mara kwa mara katika sehemu ya kaskazini mashariki ya China. Ukisafiri kutoka upande wa magharibi hadi upande wa mashariki mkoani Jilin, utaweza kuona vivutio vingi vya Ziwa Chagan, kuteleza kwenye theluhi katika mji wa Changchun, kuona matawi ya miti yenye barafu, Mlima Changbai pamoja na furaha na shughuli nyingi za theluji.

    Katika picha za ardhini zilizopigwa kwenye anga ya juu, watu wanaweza kuona kuwa mto Songhua wa upande wa kusini na mto Nenjiang wa upande wa kaskazini inakutana kwenye sehemu ya magharibi ya mkoa wa Jilin, na kuwa ziwa kubwa la Chagan lenye eneo la kilomita za mraba 420. Kila ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba, maji ya ziwa huganda kwa unene wa mita 1 hadi 2 kutoka sehemu ya juu. Wavuvi wa huko wanavua samaki kwa mbinu ya kizamani sana ya kutoboa barafu kwenye mto. Shughuli hizo zimesifiwa na wataalamu wa mambo ya mila kuwa ni utamaduni pekee wa uvuvi uliobaki kwenye dunia yetu. Njia hiyo ya kujipatia riziki imehifadhi utamaduni wa binadamu na kuwa historia ya sasa ya maisha ya watu wa makabila ya sehemu ya kaskazini ya China.


    1 2 3 4 5
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako