• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujifurahishe kwa mandhari ya theluji mkoani Jilin

    (GMT+08:00) 2009-01-12 15:30:12

    Hivi sasa kuteleza kwenye thaluji kumekuwa mchezo unaopendwa na watu wengi katika mji wa Changchun. Kila mwaka baada ya kuingia katikati ya mwezi Novemba, huonekana halaiki ya watu na vicheko kwenye sehemu mbalimbali za mchezo wa kuteleza kwenye theluji, ambapo watu hufanya mazoezi na kuonesha ustadi wao.

    Licha ya kupenda kuteleza kwenye theluji, watu vilevile wanapenda kuteleza kwenye theluji kutoka sehemu za juu zenye kimo cha mita kadhaa, zaidi ya kumi na mita kumi kadhaa kwenda chini, wakati watu wengine wanashuka chini kwa kasi wakikaa ndani ya gurudumu kubwa, sauti ya furaha inachanganyika pamoja na sauti ya mayowe.

    Mlima Changbai ni mahali pazuri zaidi pa kuangalia mandhari ya theluji na kucheza michezo ya theluji. Mlima Changbai uko sehemu ya mashariki kabisa ya mkoa wa Jilin, watu wakitaka kwenda huko kutoka mji wa Changchun, wanaweza kutumia gari, ambalo linachukua muda wa saa 6 hivi. Mlima Changbai wote ni mweupe kabisa, na ni wazi kwa watu katika majira ya baridi, hivyo watalii licha ya kuweza kuinua vichwa kuangalia milima mirefu kwenye barafu ya ziwa la Tianchi na kuoga katika madimbwi ya maji ya chemchemi moto, vilevile wanaweza kupita kwenye misitu ya ardhini huku wakiburudishwa na mandhari ya matawi ya miti yenye theluji na barafu. Watalii walisema:

    "Kwa sababu tunafika hapa kwa ndege kutoka sehemu ya joto ya Guangzhou, hivyo tunaona tofauti kubwa sana, hapa panaonekana kama ni dunia iliyosimuliwa katika hadithi."


    1 2 3 4 5
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako