Wavuvi wanapaza sauti na kuendesha farasi wanne kuzungusha gurudumu kubwa kwenye umbali wa mita mia kadhaa, ambapo wavu mkubwa unavutwa nje kutoka katika tundu la barafu, samaki waliokamatwa wanatolewa nje huku wakirukaruka kwenye barafu, watalii wengi wanawashamgilia wavuvi. Mtalii mmoja alisema:
"Nilifika hapa kwa teksi, nilitembelea sehemu nyingi za China, lakini sikuona hali kama hiyo."
Ziwa Chagan lina samaki karibu aina 70, hususan aina ya samaki mwenye kichwa kikubwa na madoa mwilini, ambao wana ladha nzuri na kujenga mwili.
Mchezo wa kuteleza kwenye theluji, ingawa siyo wa kuchangamsha sana kama shughuli za kuvua samaki kwenye mto ulioganda barafu, lakini ni mchezo unaopendwa sana na watu mkoani Jilin. Jilin ina sehemu nyingi zenye theluji zinazoweza kutumiwa kufanya mchezo wa kuteleza, ambazo zinazidi 70 kwa jumla, kwa hiyo mkoa wa Jilin unasifiwa na watu kuwa ni mahali pazuri kabisa kwa mchezo wa kuteleza kwenye theluji nchini China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |