Ziwa Chagan liko kwenye wilaya ya Guo ya zamani, ambayo iko kwenye sehemu ya kaskazini magharibi ya mkoa wa Jilin, na hivi sasa ni wilaya inayojiendesha ya kabila la Wamongolia. Wakazi wa huko wana mazoea ya kuvua samani katika majira ya baridi kwa zaidi ya miaka 1,000 iliyopita.
Kila mwaka kabla ya kuanza shughuli za uvuvi, wavuvi kwenye Ziwa Chagan, hufanya tambiko kwa ziwa na kuombea mavuno mazuri ya uvuvi na maisha mazuri ya wavuvi. Wavuvi hutoa kafara ya sukari, mchele uliokaangwa, matunda na samli, na kuchoma udi. Baada ya kuchezwa ngoma ya Chama na watawa kufanya ibada, vitu vya vilivyotolewa kafara vinatumbukizwa ndani ya matundu yaliyotobolewa kwenye barafu mtoni, hapo kiongozi wa wavuvi anasoma risala ya tambiko.
Baada ya kunywa pombe, wavuvi wanapanda kwenye magari ya farasi kwenda kuvua samaki.
Wavu unaotumiwa na wavuvi wa kuvua samaki katika Ziwa Chagan ni wavu mkubwa wenye urefu wa zaidi ya mita 3,000 na upana wa zaidi ya mita 2. mnamo saa kumi alfajiri, wavuvi wanatoboa tundu kubwa kwenye barafu, mahali palipothibitishwa na kiongozi wao, ambapo wavu unashushwa chini, baadaye yanatobolewa matundu kila baada ya mita 15 kwenye eneo lenye mita 1 za mraba, na wavu unavutwa chini ya barafu kwa fimbo yenye urefu wa mita 18 hadi 20.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |