"Tunaona hapa ni tofauti kabisa, tena ni ajabu sana, upande huu ni chemchemi ya maji baridi yenye barafu, na upande mwingine ni chemchemi ya maji moto."
Naibu mkurugenzi wa idara ya utalii ya kamati ya usimamizi ya Mlima Changbai, Bw. Meng Fanying alisema,
"Hivi sasa, magari yote yawe madogo ama makubwa yanaweza kufika katika sehemu zote zenye vivutio. Jambo lingine ni kuwa wageni wanaweza kupata chakula, vyumba vya kulala pamoja na mambo ya burudani katika sehemu hizo, tena gharama inapunguzwa kwa nusu ikilinganishwa na ile ya majira ya joto."
Bustani ya kimataifa ya kuteleza kwenye theluji ya mtelemko wa magharibi wa Mlima Changbai, ambayo ilifunguliwa mwaka uliopita, ni sehemu ya kipekee nchini na inachukua nafasi ya kwanza kwa ukubwa kwa michezo ya kuteleza kwenye thaluji katika Asia, inafanya Mlima Changbai kuwa wa kuvutia zaidi.
"Mchezo wa kuteleza kwenye theluji ni mchezo wa kuwapa watu furaha wakati wanapoteleza kwenye theluji, tena ungewapa watu furaha kubwa zaidi kwa kuvutiwa na mandhari nzuri ya kupendeza. Watu waliofika Mlima Changbai, wanaweza kupata furaha za aina zote mbili."
Kuvuta hewa safi, kusikiliza sauti ya mtiririko wa maji, na kujipumzisha vizuri katika mazingira ya pori yasiyo na makelele, watu wanajiburudisha kwa raha katika hali ya mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |