Hotuba ya Rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa viongozi wa dunia kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
Katika maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Umoja wa mataifa, na maadhimisho ya miaka 20 ya mkutano wa nne kuhusu wanawake uliofanyika Beijing, ni muhimu kwa kuitisha mkutano wa viongozi wa dunia kuthibitisha ahadi zetu kuhusu usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake, na kuweka mipango kwa ajili ya siku nzuri za baadaye...
| Kufanya kazi kwa pamoja ili Kuunda Ushirikiano Mpya wa kunufaisha pande zote na Kujenga Jumuiya ya Pamoja kwa ajili ya vizazi vijavyo -- Hotuba katika Mjadala Mkuu wa Kikao cha 70 cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Miaka sabini iliyopita, kizazi kilichopita kilipigana vita kishujaa na kushinda mapambano dhidi ya ufashisti duniani na kufunga ukurasa kwa kiza katika historia ya binadamu. Ushindi huo haukuwa rahisi. Miaka sabini iliyopita, kizazi hicho, chenye maono na mtizamo wa siku za usoni, kilianzisha Umoja wa Mataifa-mpango kamwe haukuwa umefanyika kabla. Shirika hilo la kimataifa linalowakilisha wote limeleta matumaini tumaini kwa wanadamu na kufungua ukusara wa zama mpya za ushirikiano.
|
Kuelekea uhusiano wa kunufaishana kwa maendeleo endelevu -- Hotuba iliyotolewa na Rais Xi Jinping wa China katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu
Nina furaha kubwa kuhudhuria mkutano wa leo. Ikiwa Umoja wa Mataifa unaadhimisha miaka 70, hii ni fursa muhimu nay a kipekee kwa viongozi wa dunia kukutana pamoja mjini New York kuratibu mwelekeo wa maendeleo ya baadaye. Maendeleo yanabeba matumaini na maisha halisi ya watu wa nchi zote. Inajumuisha uhalisia wa hadhi zao na haki zao. Ni katika mtazamo huo ndipo tuliweka Malengo ya Maendeleo ya Milenia miaka 15 iliyopita katika juhudi za kuboresha maisha ya mamilioni ya watu.
| China iko hapa kwa ajili ya Amani -- Taarifa kwa Mkutano wa Kilele wa Kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa
Namshukuru Rais Obama kwa juhudi zake za kuitisha mkutano huu wa kilele wa kulinda amani. Amani ni matumaini ya kawaida na ni lengo kubwa lililopo kwa kila binadamu. Ni kutokana na madhumuni ya kupata amani ndio Opresheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa zikaanzishwa. Hivi sasa zikiwa kama ni njia muhimu ya kushikilia amani na usalama duniani, operesheni hizi za kulinda amani zimeleta imani kwenye maeneo yanayokabiliwa na migogoro, na kutoa matumaini kwa wahanga wa maeneo hayo.
|