• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 13-Agusti 19)

    (GMT+08:00) 2016-08-19 18:47:32

    Mujuru asema ataungana na MDC kumuondoa Mugabe

    Aliyekuwa makamu wa rais wa Zimbabwe Joyce Mujuru anasema kuwa atafurahia kubuni muungano na chama cha upinzani cha MDC ili kumuondoa madarakani rais Robert Mugabe.

    Bi Mujuru ameviambia vyombo vya habari kwamba yuko tayari kufanya kazi na chama cha Movemnet for Democratic Change kinachoongozwa na Morgan Tsvangira na wengine kwa niaba ya raia wa taifa hilo.

    Alizindua rasmi chama chake mapema mwaka huu baada ya kufutwa kazi kama makamu wa rais kabla ya kufukuzwa katika chama tawala cha ZANU PF .

    Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 92 amesema kuwa atawania muhula mwengine katika uchaguzi ujao.

    Kumekuwa na maandamano katika wiki za hivi karibuni kuhusu hali mbaya ya kiuchumi nchini Zimbabwe.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako