• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Agusti 13-Agusti 19)

    (GMT+08:00) 2016-08-19 18:47:32

    Polisi Rwanda wamuua mshukiwa wa ugaidi

    Polisi nchini Rwanda wanasema wamempiga risasi na kumuua mshukiwa wa ugaidi katika mtaa wa kifahari wa Nyarutarama jijini Kigali.

    Mshukiwa huyo ametambuliwa kwa jina la Channy Mbonigaba kutoka Wilaya ya Rubavu Magharibi mwa nchi hiyo, aliuawa baada ya kukabiliana na Polisi kwa zaidi ya saa tatu.

    Ripoti zaidi zinasema mshukiwa huyo alikuwa amejificha ndani ya nyumba moja katika mtaa huo wakati Polisi walipoanza kukabiliana naye.

    Mbonigaba amekuwa akishukiwa kuwa miongoni mwa kundi la vijana wa Kiislamu ambalo Polisi kwa miezi kadhaa sasa wanasema limekuwa likipewa mafunzo ya kijihadi.

    Kuuawa kwa mshukiwa huyu kunakuja baada ya Muhammad Mugemangango, Naibu Imam wa Msikiti wa maarufu wa Kimironko katika Wilaya hiyo ya Rubavu kukamatwa kwa madai ya kuwapa vijana mafunzo ya kijihadi.


    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako