Serikali ya DRC yatangaza amri ya kutotoka nje usiku Beni na Butembo
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza Alhamisi hii, Agosti 18, amri ya kutotoka nje usiku katika miji ya Beni na Butembo, mashariki mwa nchi hiyo, baada ya maandamanoya Jumatano wiki hii dhidi ya serikali.
Wakazi wa miji hiyo wametakiwa kutotoka nje kuanzia saa moja usiku gadi saa kumi na mbili asubuhi. Tangazo hili limetolewa na Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani, Evariste Boshab. Hatua ambayo haikuwaridhisha wafanyabiashara. Wafanyabiasha katika mji wa Beni waliamua Alhamisi hii kufunga maduka yao katika barabara kuu ya Nyamwisi. Wafanyabiashara wanaomba kuachiwa huru kwa waandamanaji wanaozuiliwa.
Katikati mwa mji wa Beni, maduka yalifungwa Alhamisi hii Agosti 18 kwenye barabara kuu ya Nyamwisi ambapo ni moja ya meneo kulikofanyika maandamano ya Jumatano. Wafanyabiashara wameeleza kwamba bado wanaomboleza wahanga wa tukio hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |