• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 10-Septemba 16)

  (GMT+08:00) 2016-09-16 16:34:49

  Watu 17 wafariki kutokana na tetemeko la ardhi kaskazini mwa Tanzania

  Watu 17 wamefariki na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa baada ya tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 5.7 katika kipimo cha Richter kutokea jumamosi iliyopita mkoani Kagera nchini Tanzania.

  Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa jana alitembelea mkoa wa huoa kuwafariji wahanga wa tetemeko hilo na kukagua hasara iliyotokana na maafa hayo. Waziri mkuu Majaliwa amesema, serikali ya Tanzania itapeleka wataalamu kutathmini hasara iliyosababishwa na tetemeko hilo, na amesema serikali itatafuta msaada wa kiufundi kutoka kwa mashirika ya hali ya hewa ili kupima kama tetemeko litatokea tena katika siku za baadae.

  Kufuatia tetemeko hilo, China imepeleka madaktari watano mkoani Kagera, Tanzania, kusaidia kutoa matibabu kwa watu walioathiriwa na tetemeko hilo, wakiwemo madaktari wa magonjwa ya wanawake, watoto, upasuaji, na wa magonjwa ya kawaida.

  Ujumbe wa mabalozi kutoka nchi mbalimbali nchini Tanzania pamoja na jamii ya wafanyabiashara ulitoa mchango wa dola za kimarekani laki 7 na vifaa vingine vya kuwasaidia watu waliokumbwa na maafa hayo.


  1 2 3 4 5 6 7 8 9
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako