• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 10-Septemba 16)

    (GMT+08:00) 2016-09-16 16:34:49

    Zaidi ya waandishi wa habari 95 wauawa katika nchi 25 mwaka huu

    Shirika lisilo la kiserikali PEC lenye makao makuu yake mjini Geneva limesema, tangu mwaka huu uanze, zaidi ya waandishi wa habari 95 wameuawa katika nchi 25.

    Katika barua ya wazi kwa Kikao cha 33 cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea, PEC imesema usalama na ulinzi wa waandishi wa habari unaendelea kuwa mbaya katika nchi zenye vita kama vile Syria, Yemen, Iraq, Afghanistan na Libya. Barua hiyo imesema kuwa, lengo la mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari yaliyofanywa na makundi ya kigaidi na makundi mengine ni kuzuia upatikanaji wa ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

    PEC imelihimiza Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina zaidi kuhusu mauaji hao, ikisema kuwa hatua mpya zinahitajika ili kuboresha hali hiyo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako