China yatoa ripoti kuhusu maendeleo ya ulinzi wa haki za binadamu katika mfumo wa sheria
Serikali ya China imetoa ripoti kuhusu maendeleo ya ulinzi wa haki za binadamu iliyoyapata nchi hiyo katika upande wa mfumo wa sheria.
Ripoti hiyo inasema katika miaka iliyopita hasa minne iliyopita, China imejitahidi kuleta usasa katika mfumo wa utawala kwa kutunga sheria kwa njia za kisayansi, kutekeleza sheria kwa makini, na kuendesha mashitaka kwa usawa, na kulinda haki na uhuru wa wananchi kwa mujibu wa sheria.
Ripoti hiyo inasema China itaendelea kuboresha ulinzi wa haki za binadamu katika upande wa mfumo wa sheira kwa kujifunza kutoka nchi nyingine na kuzingatia hali halisi ya nchi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |