• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ( Septemba 10-Septemba 16)

    (GMT+08:00) 2016-09-16 16:34:49

    Mkutano wa viongozi wa IGAD wafanyika nchini Somalia

    Viongozi wa nchi wanachama wa Shirika la Maendeleo la Nchi za Afrika Mashariki IGAD wamemaliza mkutano wao wa siku moja mjini Mogadishu, Somalia, ambapo walitoa wito kwa nchi hiyo kufanya uchaguzi huru na wa haki.

    Viongozi hao akiwemo rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, na rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, pia wamepitisha mwongozo wa uchaguzi wa mwaka 2016 utakaotumika katika uchaguzi nchini Somalia.

    Katika Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo, viongozi hao pia wamewataka wananchi wa Somalia kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi huo, pia wameipongeza serikali ya Somalia kwa ahadi yake ya kufanya uchaguzi wa wazi, wa kuaminika, na jumuishi.

    Mkutano huo, ambao ni wa kwanza kufanyika mjini Mogadishu tangu IGAD ianzishwe mwaka 1986, pia umezitaka nchi za kanda hiyo kuendelea kushirikiana na serikali ya Somalia ili kudumisha juhudi za kuleta utulivu nchini humo.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako