• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 24-Septemba 30)

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:18:00

    2. Kifo cha Shimon Peres ni habari ambayo pia ilitawala vichwa vya habari katika wiki hiii. Viongozi wa dunia wamehudhuria mazishi ya waziri mkuu na rais zamani wa Israel, Shimon Peres. Mazishi hayo yamegubikwa na ulinzi mkali. Orodha kubwa ya viongozi wa mataifa mengine waliwasili kwaajili ya kutoa heshima zao za mwisho, wakiwemo Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, Waziri wa mambo ya nje wa Misri, Sameh Shoukry na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani. Itakuwa mara ya kwanza kwa Bw Abbas kuzuru Israel tangu 2010. Maelfu ya Waisraeli walitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Peres, ambaye maiti yake imekuwa nje ya majengo ya Bunge la Israeli, Knesset. Mazishi hayo ndiyo makubwa zaidi kuwahi kufanyika Israel tangu mazishi ya waziri mkuu Yitzhak Rabin, aliyeuawa na Myahudi 1995.

    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako