• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Septemba 24-Septemba 30)

    (GMT+08:00) 2016-09-30 18:18:00

    4. Nchini Uganda Jeshi la nchi hiyo limesema hatua sahihi zitachukuliwa ili kumwokoa askari wake mmoja aliyetekwa nyara mwaka jana na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

    Msemaji wa jeshi hilo Luteni Kanali Paddy Ankunda amesema, uongozi wa juu wa jeshi la ulinzi la Uganda unatilia maanani maisha ya askari huyo aliyetambuliwa tu kama Masasa. Jumatatu wiki hii, wapiganaji wa kundi la Al Shabaab walitoa video ya Masasa ambaye walimteka nyara baada ya kufanya shambulizi baya zaidi kwenye kambi ya jeshi ya Uganda iliyoko Janaale, kilomita 90 kusini magharibi mwa Mogadishu Septemba Mosi mwaka jana. Karibu askari 18 wa Uganda walioko kwenye kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia waliuawa kwenye shambulizi hilo. Hii ni video ya pili ambapo Masasa anaomba aokolewe.

    1 2 3 4 5 6 7
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako