• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 15-Oktoba 21)

    (GMT+08:00) 2016-10-21 19:05:46

    Aliyekuwa Makamu wa DRC Jean-Pierre Bemba akutwa na hatia ya kuhonga mashahidi

    Mahakama ya Kimataifa ICC imemkuta aliyekuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba na hatia ya kuwahonga mashahidi katika kesi inayomkabiloi ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

    Jumatano hii Bw Bemba amehukumiwa kwa kuwashaiwshi mashahidi baada ya kupewa khongo na kubadilisha ushahidi katika kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa KIvita.

    Washirika wake wanne wa karibu pia wameutwa na hatia.

    Itafahaamika kwamba Mwezi Machi mwaka huu Bemba alipatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadmu aliotekeleza nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kati ya mwaka 2002 na 2003. Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ilimuhukumu kifungo cha miaka 18 jela.

    Hata hivyo Jean-Pierre Bemba alipinga uamuzi huo na aliamua kukata rufaa.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako