• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Oktoba 15-Oktoba 21)

    (GMT+08:00) 2016-10-21 19:05:46

    Waziri mkuu wa Uingereza ahudhuria mkutano wa kwanza wa EU

    Waziri mkuu wa Uingereza,Theresa May, yupo mjini Brusels nchini Ubelgiji kwa mkutano wake wa kwanza wa Umoja wa Ulaya tangu kuingia madarakani katika kura ya Uingereza kujitenga na Muungano wa Ulaya.

    Amesema atawaambia wenzake kwamba Uingereza itatoa mchango wake kikamilifu hadi kuondoka kwake, na utakuwa imara na wenye kutegemea washirika baadae.

    Lakini Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, ameonya kuwa kama Bi May alitaka kujiondoa kikamilifu katika Umoja wa ulaya, kungekuwa vigumu kukubaliana katika miezi ya mbeleni.

    Taarifa zinasema serikali ya Bi May ina mgawanyiko juu ya biashara gani Uingereza inapaswa kulenga.

    Uingereza inatarajiwa kuanza mchakato wa kujiondoa rasmi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka ujao.


    1 2 3 4 5 6 7 8 9
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako