• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 5-Novemba 11)

  (GMT+08:00) 2016-11-11 19:21:42

  Donald Trump achaguliwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani

  Mgombea Urais kwa Chama cha Republican Donald Trump ameshinda uchaguzi wa Urais nchini humo na kumbwaga mgombea wa Democrat Hillary Clinton ambaye wengie walidhania angetwaa ushindi.

  Bi. Clinton amekubali kushindwa kwenye uchaguzi huo wa kihistoria na kuwataka wamarekani wampe Trump nafasi ya kuongoza.

  Hata hivyo kumekuwa na maandamano katika miji mbalimbali nchini Marekani kupinga ushindi wa Donald Trump

  Wengi wamekusanyika nje ya jumba maarufu la rais huyo mteule Trump Tower mjini New York wakipaza sauti zao dhidi ya msimamo wa Bw Trump kuhusu sera za uhamiaji, mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump.

  Tayari Rais mteule huyo wa Marekani Donald Trump na Rais anayeondoka madarakani Barack Obama wakikutana katika ikulu ya White House.

  Wawili hao wamesema watafanya kazi pamoja.

  Trump ambaye sasa atakuwa rais wa 45 wa Marekani amesema atapunguza kodi na kufanya mageuzi ya sekta ya huduma za afya kwa kuachana na mfumo uliowekwa na Barack Obama.

  Pia amesema atabadili haraka sheria juu ya uhamiaji, Hizo ni miongoni mwa hatua tatu muhimu alizoahidi kwenye kampeni zake za Urais.


  1 2 3 4 5 6 7 8
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako