• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 5-Novemba 11)

    (GMT+08:00) 2016-11-11 19:21:42

    Rwanda kuwachunguza maofisa wa Ufaransa wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari

    Rwanda itawafanyia uchunguzi maofisa wa Ufaransa wanaotuhumiwa kupanga mauaji ya kimabari ya mwaka 1994 yaliyosababisha vifo vya watu milioni 1 nchini humo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Bibi Louise Mushikiwabo amesema mchakato wa kisheria dhidi ya maofisa wa Ufaransa wanaotuhimiwa utaanza kwa uchunguzi wa kina.

    Bibi Mushikiwabo amesema, watatumia njia zao kutekeleza mchakato wa kisheria dhidi ya maofisa hao nchini Ufaransa wenye kesi za kujibu. Wataiomba serikali ya Ufaransa kuwapatia njia kukutana na baadhi ya watu.

    Amesisitiza kuwa Ufaransa ilituma washauri wa kisiasa na kijeshi kwa serikali iliyokuwa inatawala Rwanda wakati mauaji ya kimbari yalipotokea mwaka 1994.

    Mwezi uliopita kamati ya taifa ya kupambana na mauaji ya kimbari CNLG ilitoa orodha ya majina ya wanajeshi 22 wa ngazi ya juu wanaotuhumiwa kusaidia kwa makusudi mpango wa mauaji ya kimbari.


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako