• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii (Novemba 5-Novemba 11)

    (GMT+08:00) 2016-11-11 19:21:42

    Kenya yaondoa askari wake nchini Sudan Kusini

    Kundi la kwanza la wanajeshi wa kulinda amani wa Kenya waliokuwa nchini Sudan Kusini chini ya Umoja wa Mataifa limerejea nyumbani wiki hii.

    Serikali ya Kenya iliytangaza awali kwamba itaondoa askari wake 1,000 ambao ni sehemu ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kufuatia kufutwa kazi kwa kamanda wake.

    Hatua hiyo inakuja baada ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kusema uamuzi wa Kenya kujitoa kwenye kikosi hicho ni kupinga ukiukaji wa hadhi ya askari wa Kenya.

    Rais Kenyatta amesema kuwa Umoja wa Mataifa ulichukua hatua isiyo ya kinidhamu wakati ilipombadilisha Luteni Jenerali Johnson Ondiek ambaye alikuwa kiongozi wa Kikosi hicho nchini Sudan Kusini.

    Pia amesema kuwa Umoja wa Mataifa haukuheshimu mamlaka ya Kenya wakati inachukua uamuzi huo, ambao Kenya imeujibu kwa kuwaondoa askari wake kutoka kwenye kikosi hicho.

    Rais Kenyatta amesema, Kenya itaendelea kuiunga mkono Sudan Kusini katika ngazi ya pande mbili na pia kupitia Umoja wa Afrika, Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la Kikanda, na Jumuiya ya Afrika Mashariki


    1 2 3 4 5 6 7 8
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako